Zaburi 117

Kumsifu Mungu

1 Enyi mataifa yote, msifuni Mwenyezi-Mungu!

Enyi watu wote mhimidini!

2 Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu;

uaminifu wake Mwenyezi-Mungu wadumu milele!

Msifuni Mwenyezi-Mungu!