Kumtumainia Mungu kwa utulivu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1 Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi;
mimi si mtu wa majivuno.
Sijishughulishi na mambo makuu,
au yaliyo ya ajabu mno kwangu.
2 Ila nafsi yangu imetulia na kuwa na amani,
kama mtoto mchanga alivyotulia na mama yake;
ndivyo nafsi yangu ilivyo tulivu.
3 Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu,
tangu sasa na hata milele.