Mungu mfalme
1 Mwenyezi-Mungu anatawala;
amejivika fahari kuu!
Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu!
Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe.
2 Kiti chako cha enzi ni imara tangu kale;
wewe umekuwapo kabla ya nyakati zote.
3 Vilindi vimetoa sauti, ee Mwenyezi-Mungu;
naam, vimepaza sauti yake,
vilindi vyapaza tena mvumo wake.
4 Mwenyezi-Mungu ana enzi kuu juu mbinguni,
ana nguvu kuliko mlio wa bahari,
ana nguvu kuliko mawimbi ya maji.
5 Ee Mwenyezi-Mungu, maagizo yako ni thabiti;
nyumba yako ni takatifu milele na milele.