Wimbo wa shukrani
1 Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
2 Mshukuruni Mungu wa miungu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
3 Mshukuruni Bwana wa mabwana;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
4 Ndiye peke yake atendaye makuu ya ajabu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
5 Ndiye aliyeziumba mbingu kwa hekima;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
6 Ndiye aliyeitengeneza nchi juu ya vilindi vya maji;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
7 Ndiye aliyeumba jua, mwezi na nyota;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
8 Jua liutawale mchana;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
9 Mwezi na nyota vitawale usiku;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
10 Ndiye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
11 Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
12 Kwa mkono wake wenye nguvu na enzi;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
13 Ndiye aliyeigawa Bahari ya Shamu sehemu mbili;
kwa maana fadhili zake zadumu milele,
14 akawapitisha watu wa Israeli humo;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
15 Lakini akawazamisha humo Farao na jeshi lake;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
16 Ndiye aliyewaongoza watu wake jangwani;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
17 Ndiye aliyewapiga wafalme wenye nguvu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
18 Akawaua wafalme maarufu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
19 akamuua Sihoni, mfalme wa Waamori,
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
20 na Ogu, mfalme wa Bashani;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
21 Akachukua nchi zao akawapa watu wake;
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
22 ziwe riziki ya Israeli, mtumishi wake;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
23 Ndiye aliyetukumbuka wakati wa unyonge wetu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
24 akatuokoa kutoka maadui zetu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
25 Ndiye akipaye kila kiumbe chenye uhai chakula;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
26 Mshukuruni Mungu wa mbinguni;
kwa maana fadhili zake zadumu milele!