Zaburi 134

Msifuni Mungu

(Wimbo wa Kwenda Juu)

1 Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote,

enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.

2 Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu,

na kumtukuza Mwenyezi-Mungu!

3 Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni;

yeye aliyeumba mbingu na dunia.