Sala dhidi ya maadui wa Israeli
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu
Kila mtu katika Israeli na aseme:
2 “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu,
lakini hawakufaulu kunishinda.
3 Walinijeruhi vibaya mgongoni mwangu,
wakafanya kama mkulima anayelima shamba.
4 Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu;
amezikata kamba za hao watu waovu.”
5 Na waaibishwe na kurudishwa nyuma,
wote wale wanaouchukia mji wa Siyoni.
6 Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba,
ambazo hunyauka kabla hazijakua,
7 hakuna anayejishughulisha kuzikusanya,
wala kuzichukua kama matita.
8 Hakuna apitaye karibu atakayewaambia:
“Mwenyezi-Mungu awabariki!
Twawabariki kwa jina la Mwenyezi-Mungu!”