Usalama wa watu wa Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni,
ambao hautikisiki bali wabaki imara daima.
2 Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima,
ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake,
tangu sasa na hata milele.
3 Waovu hawataendelea kutawala nchi ya waadilifu;
wasije waadilifu nao wakafanya maovu.
4 Ee Mwenyezi-Mungu, uwe mwema kwa watu wema,
kwa wale wanaozitii amri zako.
5 Lakini wanaogeuka na kufuata njia zao mbaya
uwakumbe pamoja na watenda maovu.
Amani iwe na Israeli!