Zaburi 91

Mungu mlinzi wetu 1 Anayekaa chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu, anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu, 2 ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu;…

Zaburi 92

Wimbo wa kumsifu Mungu (Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato) 1 Ni vema kukushukuru, ee Mwenyezi-Mungu, kuliimbia sifa jina lako, ee Mungu Mkuu. 2 Ni vema kutangaza fadhili zako asubuhi,…

Zaburi 93

Mungu mfalme 1 Mwenyezi-Mungu anatawala; amejivika fahari kuu! Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu! Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe. 2 Kiti chako cha enzi ni imara tangu kale; wewe umekuwapo kabla…

Zaburi 94

Mungu hakimu wa wote 1 Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwenye kulipiza kisasi, ewe Mungu mlipiza kisasi, ujitokeze! 2 Usimame, ee hakimu wa watu wote; uwaadhibu wenye kiburi wanavyostahili! 3 Waovu wataona…

Zaburi 95

Utenzi wa kumsifu Mungu 1 Njoni tumwimbie Mwenyezi-Mungu, tumshangilie mwamba wa wokovu wetu! 2 Twende mbele zake na shukrani; tumshangilie kwa nyimbo za sifa. 3 Maana Mwenyezi-Mungu, ni Mungu mkuu;…

Zaburi 96

Mungu mfalme na hakimu 1 Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya! Mwimbieni Mwenyezi-Mungu, ulimwengu wote! 2 Mwimbieni Mwenyezi-Mungu na kulisifu jina lake. Tangazeni kila siku matendo yake ya wokovu. 3 Yatangazieni mataifa…

Zaburi 97

Mungu mtawala mkuu 1 Mwenyezi-Mungu anatawala! Furahi, ee dunia! Furahini enyi visiwa vingi! 2 Mawingu na giza nene vyamzunguka; uadilifu na haki ni msingi wa utawala wake. 3 Moto watangulia…

Zaburi 98

Mungu mtawala wa dunia yote 1 Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu! Mkono wake hodari, mkono wake mtakatifu umempatia ushindi. 2 Mwenyezi-Mungu ameonesha ushindi wake; ameyadhihirishia…

Zaburi 99

Mungu mtawala mkuu 1 Mwenyezi-Mungu anatawala, mataifa yanatetemeka! Ameketi juu ya viumbe vyenye mabawa, nayo dunia inatikisika! 2 Mwenyezi-Mungu ni mkuu katika Siyoni; ametukuka juu ya mataifa yote. 3 Wote…

Zaburi 100

Wimbo wa sifa (Zaburi ya shukrani) 1 Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote! 2 Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe! 3 Jueni kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu. Yeye ndiye…